Darasa la 1 · Kiswahili · Kusikiliza na Kuzungumza (Matamshi Bora)
Tamka kila herufi na silabi wazi. Herufi mbili zinaweza kutoa sauti moja: ch (chai), sh (shule), ng' (ng'ombe), ny (nyumba), th (thelathini), dh (dhahabu). Sema polepole na kwa sauti inayosikika.