Darasa la 3 · Kiswahili · Kuzungumza (Heshima na Adabu)
Wazee tunawasalimia kwa 'Shikamoo' na wao hujibu 'Marahaba'. Tunasema 'tafadhali', 'asante', 'samahani', 'pole', 'karibu', 'kwaheri'. Tunasikiliza bila kukatiza. Tunawasaidia wazee kubeba mizigo na kuvuka barabara.