Mimea ina mizizi, shina, majani, maua na matunda. Mizizi hufyonza maji kutoka ardhini na kushikilia mmea. Majani hutengeneza chakula kwa kutumia mwanga wa jua. Matunda ni kama embe, chungwa, ndizi, papai, nanasi na parachichi. Matunda yana vitamini na hutupa afya.