Kitenzi ni neno linaloeleza kitendo. Wakati uliopo: -na- (ninasoma). Wakati uliopita: -li- (nilisoma). Wakati ujao: -ta- (nitasoma). Wakati timilifu: -me- (nimesoma). Viambishi vya nafsi: ni- (mimi), u- (wewe), a- (yeye), tu- (sisi), m- (ninyi), wa- (wao).