Maadili ni tabia njema zinazokubalika katika jamii. Mifano ni uaminifu, heshima, ukarimu, uwajibikaji na uvumilivu. Tabia mbaya ni wizi, udanganyifu, matusi na uvivu. Mtu mwenye maadili huishi vizuri na wengine. Wazazi na walimu hutufundisha maadili.