Darasa la 6 · Kiswahili · Sarufi (Kauli ya Kutendea)
Kauli ya kutendea huonyesha kitendo kinafanywa kwa ajili ya mtu au kwa kutumia kitu. Vitenzi huongezewa -i- au -e-: pika - pikia; andika - andikia; soma - somea; enda - endea; leta - letea; fungua - fungulia; cheza - chezea.