Mshikamano wa kitaifa ni umoja wa Wakenya licha ya tofauti za kabila, dini na lugha. Alama zinazotuunganisha ni bendera, wimbo wa taifa, nembo na lugha ya taifa Kiswahili. Sherehe za kitaifa ni Siku ya Madaraka (1 Juni), Siku ya Mashujaa (20 Oktoba) na Siku ya Jamhuri (12 Desemba). Tunaishi kwa amani na kuvumiliana.