Wanyama wa majini wanaishi baharini, mitoni na maziwani. Mifano: samaki, papa, pomboo, nyangumi, kaa, kobe, pweza na mamba. Samaki hupumua kwa matamvua (gill), ilhali nyangumi na pomboo ni mamalia wanaopumua kwa mapafu. Samaki ni chakula chenye protini. Tunahifadhi maji yasichafuliwe.