Darasa la 7 · Kiswahili · Sarufi (Aina za Sentensi)
Sentensi sahili ina kishazi kimoja huru: Juma anasoma. Sentensi ambatano ina vishazi huru viwili au zaidi vilivyounganishwa na na, lakini, au: Juma anasoma na Amina anaandika. Sentensi changamano ina kishazi huru na kishazi tegemezi: Juma anayesoma ni mwerevu.