Mlo kamili una makundi matano ya vyakula: vya wanga (ugali, wali, viazi), protini (nyama, samaki, maharagwe, mayai), vitamini na madini (matunda na mboga), mafuta na maji. Lishe duni husababisha utapiamlo kama kwashakoo na marasmasi. Tunakula kwa kiasi na kuzingatia usafi wa chakula.