Kishazi huru kina maana kamili peke yake: Juma anasoma. Kishazi tegemezi hakijitoshelezi: ambaye ni mwerevu; anayesoma; aliyefika; ukisoma; alipofika. Kishazi tegemezi cha kirejeshi hutumia -o-; cha masharti hutumia -ki- au -ngali-; cha wakati hutumia -po-.